Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 11:04 pm

NEWS: RAIA 115 WAMERIPOTIWA KUNYONGWA NA MAMLAKA ZA NDANI BURKINAFASO

Ripoti ya Shirika la Kimataifa la kutetea haki za Binadamu la Human Rights Watch limetoa taarifa kuwa, maafisa usalama nchini Burkina Faso wamewauwa kwa kuwanyonga raia wa kawaida 115 katikati mwa mwaka 2018.

Related image

Imeelezwa kuwa, mauaji haya yalitokea wakati wa operesheni dhidi ya makundi ya kijihadi nchini humo ambayo yamesababisha ukosefu wa usalama.

Lakini Serikali ya Burkina Faso haijakubali wala kukanusha ripoti hii lakini, imekuwa ikikanuisha ripoti kama hizi katika siku zilizopita na kutetea maafisa wake wa usalama, kwa kufanya kazi kubwa ya kupambana na ugaidi.

Image result for Human right watch Burkina Faso Killed 115 people

Mauaji hayo yote yanaelezwa, yalitokea Kaskazini mwa nchi hiyo karibu na nchi ya Mali na Niger kati ya Aprili 2018 hadi Januari 2019.

Corinne Dufka Mkuu wa Human Rights Watch kwenye ukanda wa Sahel amesema, kuwa mauaji hayo yamesababisha raia wengi kuendelea kuishi kwa wasiwasi.

Burkina Faso imetangaza hali ya hatari katika majimbo kadhaa kutokana na vita dhidi ya ugaidi kwa usaidizi wa mataifa ya Magharabi hasa Ufaransa.