- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: RAFIKI WA BOBI WINE AFARIKI DUNIA BAADA YA KUTEKWA NA WASIOJULIKANA
Rafiki wa karibu wa mwanamuziki na mbunge wa upinzani Ribert Kyagulanyi maarufu kama Bobi Wine, Allinda Michael, maarufu kama Ziggy Wine, amefariki dunia kutokana na majeraha, baada ya kutekwa na kupigwa na watu wasiojulikana, jijini Kampala nchini Uganda.
Ziggy Wine alitekwa wiki iliyopita na alipatikana Jijini Kampala siku tatu baadae (Jumamosi ya wiki iliyopita) akiwa ameng’olewa kucha na jicho moja.
Ziggy Wine alikuwa ni mmoja wasanii waliochini ya mwavuli wa People’s Power unaoongozwa na Bobi Wine.
''Jana usiku ndugu yangu, rafiki na msanii mwenza Ziggy Wine alifariki katika hospitali ya Mulago'', Bobi Wine alichapisha katika ukurasa wake wa akaunti ya Twitter.
"Our friend Ziggy Wine could not make it. He passed on last night- succumbing to injuries sustained after a horrendous encounter with kidnap & torture. Very painful! He joins other countless Ugandans. As we mourn him, we resolve to work even harder to end this. Rest well brother " ameandika Bobi kwenye ukurasa wake wa Twitter
Sababu za kutekwa msanii huyo bado hazijajulikana na jeshi la polisi nchini humo limeahidi kuwatafuta watekaji hao kwa udi na uvumba.
Kufuatia tukio hilo, Wasanii kibao akiwemo Jose Chameleone wameomboleza msiba huo na kuahidi kutafuta suluhu ya kukomesha vitendo hivyo vya utekaji.