- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: QATAR YAUNGWA MKONO NA NCHI MBILI TAJIRI
Istanbul: Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amekataa madai ya nchi za Kiarabu kuitaka Uturuki kuondoa wanajeshi wake kutoka Qatar, yakiwa ni miongoni mwa masharti mengine kadhaa ambayo Marekani imeyataja kuwa ni "vigumu kutekelezeka."
Akizungumza baada ya houba ya sikukuu ya Eid al-Fitr katika sala ya asubuhi mjini Istanbul, Erdogan amesema madai hayo ya nchi za Kiarabu ya kuitaka Uturuki kuwaondoa wanajeshi wake yamekosa heshima na kuongeza kwamba nchi yake haihitaji ruhusa ya nchi nyingine wakati wa kufanya makubaliano yake ya ushirikiano wa ulinzi.
"Tunakubali na kufahamu mtazamo wa Qatar dhidi ya orodha ya masharti hayo 13. Tunatambua kwamba njia hii ya madai 13 ni kinyume na sheria za kimataifa kwa sababu huwezi kushambulia au kuingilia nchi huru kulingana na sheria za kimataifa," amesema Recep Tayyip Erdogan.
Kwa upande wake Rais wa Iran Hassan Rouhani pia amesema jana kwamba anaiunga mkono Qatar katika kukabiliana na hasimu wa Iran - Saudi Arabia - pamoja na washirika wake kadhaa, na kusema kwamba kitendo cha "kuizingira Qatar hakikubaliki.