- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: QATAR YATENGWA NA MATAIFA 4 YA KIARABU
Doha, Nchi nne kutoka kwenye ukanda wa kiarabu wamekata uhusiano wao kidiplomasia na Qatar kwa madai ya kufadhili ugaidi Duniani,Saudi Arabia, Misri, Bahrain na milki ya nchi za kiarabu zimfunga ubalozi wake dhidi ya nchi hiyo.
Qatar ni nchi inayo onekana kuwa inaunga mkono makundi ya kigaidi likiwemo kundi la Muslim Brotherhood lililokuwa na makao makuu yake nchini Misri
Nchini Saudi Arabia kumeripotiwa kuwa imefunga mipaka yake na kusitisha usafiri wa ardhini, baharini na angani kwenda Qatar, Shirika moja nchini Saudia
Lilinukuu maafisa wakisema kuwa hatua hiyo ni ya kulinda usalama wa nchi kutokana na hatari za ugaidi na itikadi kali.
Misri nayo imefunga anga zake na bandari kwa Qatar, kwa mujibu wa wizara ya mashauri ya nchi kigeni.,
Milki ya nchi za kiarabu imewapa wanadiplomasia wa Qatar saa 48 kuondoka nchini humo.
Abu Dhabi inaishutumu Qatar kwa kufadhili ugaidi na itikadi kali.
Shirila la taifa la habari nchini Bahrain nalo limesema kuwa nchi hiyo inataka uhusiano na Qatar kwa kuvuruga usalama wake na kuingilia ndani masuala yake ya ndani.