- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: PSPF KULIPA WASTAAFU 9,552
DODOMA: KATIKA mwaka wa Fedha 2017/18 mfuko wa Hifadhi ya jamii (PSPF) umatarajia kuwalipa wastaafu 9,552 jumla ya mafao yanayofikia kiasi cha sh.trilioni 1.3.
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi mkuu wa PSPF,Adam Mayingu, alipokuwa akitoa hotuba yake kwa mgeni rasimi ambaye alikuwa ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI,Selemani Jafo.
Mayingu akitoa hotuba hiyo katika semina ya wanachama wa mfuko huo ambao wanatarajia kustaafu amesema kwa sasa mfuko huo unaongoza kwa kuwa na wanachama wengi.
Mbali na kuwa na wanachama wengi Mayingu amesema baada ya kuona wastaafu wanapata shida kwa kushindwa kutumia vyema mafao yao uongozi wa PSPF umeamua kuanzisha semina kwa watumishi wa Umma ambao ni wastaafu watarajiwa.
Amesema mfuko wa PSPF unahudumia wanachama 40,3605 wastaafu na wategemezi 81,020 ambao kwa kiasi kikubwa ni watumishi wa Umma wakiwemo walimu,askari polisi na askali magereza.
Aidha amesema kuwa wachangiaji kwa mpango wa hiari mfuko una wanachama takribani 90,000.
“Hii ni kuhakikisha kuwa mfuko unatekeleza kwa vitendo juhudi za serikali za kuhakikisha kuwa wananchi wengi zaidi wanafaidika na mfumo wa hifadhi ya jamii nchini” alisema.
“Tathimini ya mfuko tangu uanze kulipa mafao umeisha lipa kiasi cha sh.trilioni 4.2,mfuko umetathimini kiasi cha mafao yanayolipwa kila mwaka na kuona haja ya kuandaa mpango wa mafunzo maalum kwa ajili ya wanachama wake wanaotarajia kustaafu ndani ya miaka miwili ijayo” alisema Mayingu.
Naye Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais –TAMISEMI,Selemani Jafo amewataka wastaafu wote kuhakikisha wanatumia fedha zao za mafao kwa lengo kujiwekea akiba.
Jafo amesema kuwa wapo wastaafu wengi ambao baada ya kupata fedha zao za mafao wamekuwa masikini au wamekufa kutokana na kutumia vibaya fedha zao za mafao.
“Wapo wastaafu ambao walipokea mafao yao kwa wakati mmoja na kuziona fedha zao kuwa ni nyingi na kujikuta wananunua magari ambayo baada ya miezi mitatu gari linaharibika na kumfanya mstaafu kuchanganyikiwa.
“Wapo wastaafu wengi ambao wamepata magonjwa ya kupooza kutokana fedha zao za kumalizika bila kufanya kazi yoyote ya maana jambo ambalo linawatesa wastaafu” alisema Jafo.