Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 1:31 am

NEWS: PROF.NDALICHAKO: MARUFUKU WANAFUNZI KUJIHUSISHA NA MAPENZI


DODOMA: WAZIRI wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia Profesa JOYCE NDALICHAKO amewataka wanafunzi wa kike wa shule za msingi na sekondari kutojihusisha katika mahusiana ya mapenzi wakiwa shuleni na badala yake wajikite katika masomo kwani ndio ufunguo wa maisha yao.

Akizungumza katika siku ya Elimu kitaifa Jjana ambayo ilifanyika katika shule ya sekondari Msalato iliyopo Manispaa ya Dodoma Profesa NDALICHAKO amesema,kitendo cha watoto hao kuanza mapenzi wakiwa shuleni kinaweza kusababisha kukatisha masomo na ndoto zao za baadaye maishani.



Alisema kuwa lengo la serikali ni kuhakikisha kuwa inatoa elimu bila malipo hivyo kila mtu ahakikishe kuwa mwanafunzi anapata elimu iliyobora.

Hata hivyo alisema serikali imetunga sheria kali ya kuwabana wale wote wenye nia ya kukatisha masomo kwa watoto ambayo muhusika atatumikia kifungo cha miaka 30 jela, huku akiwataka wazazi kushirikiana na serikali katika kuwashughulikia wahalifu hao.



Hata hivyo Prof. Ndalichako akatoa wito wa vijana shuleni huku wahamasisha waalimu kuboresha vitengo vya ushauri nasaha kwa wanafunzi wao.


Kwa upande wake katibu mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Leonard Akwilapo alisema kuwa sherehe hizo ni maalumu kwa ajili ya kuzipongenza shule na wanafunzi waliofanya vizuri katika mitihani yao ya kitaifa ya darasa la saba, kidato cha nne pamoja na kidato cha sita .

Katika maadhimisho hayo ya siku elimu zawadi mbalimblai zilitolewa kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari waliofanya vizuri katika mitihani yao kwa mwaka 2016 ambapo jumla ya shule 2,772, za msingi 1903 ,sekondari 869 zimepatiwa zawadi huku shule 40 zikiwemo 14 za msingi na sekondari 16 zimepokea zawadi kwa niaba ya shule nyingine.