Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 6:57 am

NEWS: PROF.MUHONGO AISHUKIA MIKATABA YA MADINI ATAKA IRUDIWE UPYA.

Dodoma: SERIKALI imesema bado baadhi ya mikataba ya madini inaupungufu mkubwa na hivyo kama kuna uwezekano wa kuangaliwa upya ifanyanyike hivyo.

Kauli hiyo Imetolewa na Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo wakati akizindua Bodi yamadini na gesi (PURA) mjini hapa.

Amesema kumekuwa na mikataba ambayo ni mibovu hata yeye ambaye si mwanasheria anaiona hivyo.

“ Mikataba yetu mingine ni mibovu na kama kuna uwezekano wa kuipitia upya ifanyika hivyo kwani hata mimi ambaye si mwanasheria nikisoma naiona siyo mizuri’’ alisema.

Kutokana na hali hiyo Waziri huyo amesema wakati umefika sasa kwa watalaamu mbalimbali kuandika mikataba mizuri ya madini na gesi kujitokeza na kuilinda rasilimali za taifa ambazo ni pamaoja na madini na gesi.

Amesema si kweli kuwa Tanzania haina watalaamukuandika mikataba mizuri yenye maslahi kwa taifa lakini hawajitokezi na kuweka mikataba mizuri.

“ Watalaamu mpo kama nyinyi lakini tunashangaa kusikia mikataba ni mibovu sasa tumieni utalaam wenu vizuri’’ alisema.

Aidha aliwataka wajumbe hao wa bodi kutotumia vibaya kazi waliowepa kwa kuomba rushwa kutoka kwa wamiliki wa makampuni yatakayofanya kazi hizo za madini na gesi.

“ Hii suala la kuharikwa katika ‘dinner’ kila ukimwona mwekezaji na yeye yupo huyo tukimgundua tunamuondoa katika bodi,,’’ amesema

.Pia amewataka watanzania kuondokana na utamaduni wa kulalamika kuwa wanaibiwamadini na wawekezaji.

Amesema serikali imejipanga kuhakikisha kuwa rasimili zake zinalindwa kwa kadri inavyowezekana .