- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
News: Prof. Muhongo ameitaka bodi kuhakikisha inasimamia zaidi ubora wa vifaa vya umeme
Dodoma: Waziri wa Nishati na Madini,Prof.Sospiter Muhongo Ameiagiza bodi mpya ya wakurugenzi wa Wakala wa Nishati ya Umeme Vijijini (REA) kuwakaguwa wakandarasi wote ambao wamepata tenda ya usambazaji wa umeme vijijini.
Akizungumza na wajumbe wapya wa Bodi mpya REA Prof,Muhongo amesema bodi hiyo inatakiwa kuwa na malengo mapana kwa ajili ya kuhakikisha umeme unawafikia wananchi kwa kiwango kikubwa.
Katika kuhakikisha umeme unakuwa kichocheo cha maendeleo ni vyema umeme huo ukawekewa katika taasisi mbalimbali ili kuwapatia umeme.
“Sasa katika kutekeleza umeme unakuwa kichocheo,ni vyema umeme usivuke taasisi mbalimbali kama vile, shule zote za sekondari na shule za msingi,zahanati hospitali,mashamba makubwa na katika sehemu za kibiashara”amesema Prof Muhongo.
Katika uzinduzi huo Prof.Muhongo, ameitaka bodi hiyo kuhakikisha inasimamia zaidi ubora wa vifaa vya umeme ambavyo vina ubora.
“Nawaagiza nyie bodi kuhakikisha mnaponunua vifaa vya umeme kuhakikisha vinakuwa na ubora na vinavyozalishwa” amesema Prof Muhongo.
Pamoja na hayo ameyataka makampuni yote ya kutoka nje ya nchi ambayo yanafanya kazi ndani ni lazima kuwa na wakandarasi wadogo wa ndani na si vinginevyo.
“Haiwezekani kwa mfano nguzo za Umeme zinapatikana, hapa Iringa, lakini unaweza kushanga eti nguzo zinaagizwa kutoka Afrika kusini na maeneo mengine”amesema.