- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: PROF. LIPUMBA AWAOMBA WALIOIHAMA CUF KUREJEA
Kagera. Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) nchini Tanzania, Profesa Ibrahim Lipumba amewasihi wanachama wote waliokihama chama hicho akiwemo mbunge wa Bukoba Mjini (Chadema), Wilfred Lwakatare warejee kwenye chama hicho, huku akisema chama hicho kimeundwa kwa misingi ya haki na Usawa.
Profesa Lipumba ametoa kauli hiyo leo Jumatano Oktoba 23, 2019 katika kongamano lililohusisha viongozi wa wilaya, kata, matawi na wagombea wa serikali za mitaa kutoka wilaya ya Bukoba Mjini.
"Lwakatare ni kijana wangu wa siku nyingi nilisikitika sana alivyohamia Chadema lakini bado tunaheshimiana na kuzungumza na kama akitaka kurudi CUF maamuzi ni yake.β
"Nazungumza kwa ujumla wote waliohama CUF kwa sababu moja au nyingine na kwenda vyama vingine warejee kwenye chama chao,β amesema Profesa Lipumba.
Huku akieleza namna CUF ilivyojengwa katika msingi wa haki na usawa, Profesa Lipumba amesema, βkwa misingi hiyo tunaomba wanachama wote warejee. Tunawakaribisha watakuwa na haki kama wanachama wengine.β