- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: PROF. LIPUMBA ALISHANGAA BUNGE KUTOFANYA KAZI NA CAG
Dar es Salaam: Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba ameshangazwa na uamuzi wa Bunge wa kutofanya kazi na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad kwa madai ya Kulidhalilisha Bunge baada ya kuliita Bunge hilo ni dhaifu.
Kauli hiyo ya Prof. Lipumba ameitoa leo mara baada ya kufanya mahojiano na MCL Digital leo Alhamisi Aprili 4, 2019 amesema ripoti za CAG ni nyenzo muhimu katika kuhakikisha Bunge linaisimamia vyema Serikali. “Nimeshtushwa na uamuzi wa Bunge" amesema Lipumba
"Ripoti za CAG ni muhimu sana na jukumu la Bunge ni kusimamia Serikali sasa, utasimamiaje au kuiwajibisha Serikali bila ripoti za CAG,”amesema Profesa Lipumba. Amesema ni vyema busara ikatumika katika suala hilo na kwamba Profesa Assad ni mtu makini, mwenye uwezo mkubwa na mwadilifu katika utendaji wake. “Ninamjua vizuri huyu (Profesa Assad), alikuwa mwanafunzi wangu na mtu mwenye heshima sana. Sioni jambo la kukuza kwa sababu yale yalikuwa ni mahojiano tu" amesema Prof Lipumba
Juzi April 2, 201 Kamati ya maadili ilisema imemtiani hatiani CAG kutokana na kauli yake kwamba kutofanyiwa kazi ripoti za ofisi yake kunatokana na udhaifu wa chombo hicho cha kutunga sheria.