- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: PROF. LIPUMBA AJIPANGA UPYA KUUNDA TENA BODI YA WADHAMINI YA CUF
Chama Cha Wananchi (CUF) upande wa Mwenyekiti wa chama hicho anayetambulika na Msajili wa Vyama Vya Siasa nchini, Profesa Ibrahim Lipumba, wamesema wanajipanga upya kuitisha kikao cha baraza kuu la chama hicho ili kuunda wajumbe wa bodi mpya ya wadhamini baada ya mahakama kuu ya Tanzania kutengua Uteuzi wa bodi mpya ya wadhamini iliyoundwa na mwenyekiti huyo.
Akizungumza na wanachama wa chama cha CUF upande wa Lipumba, Mkurugenzi wa Habari wa CUF, Abdul Kambaya alisema wameukubali uamuzi wa Mahakama Kuu na wapo kwenye mchakato wa vikao vya juu vya taifa waweze kufanya uamuzi ikiwamo kuteua wajumbe kama mahakama ilivyoagiza.
“Tupo kwenye mchakato wa kuitisha kikao cha Baraza Kuu ambako muda siyo mrefu tutateua majina ya bodi ya wadhamini na kuwapitisha.
“Kikao hicho pia kitashirikisha viongozi wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kama sheria inavyotutaka tuweze kuwa na bodi bora itakayosimamia shughuli za chama,” alisema Kambaya.
Mkurugenzi huyo wa Habari upande wa Lipumba, alisema katika kipindi hiki ambacho wako kwenye uchaguzi wa ndani wa chama hicho, watahakikisha wanapata bodi mpya mapema iwezekanavyo jambo ambalo linaweza kusaidia shughuli nyingine za chama kuendelea.