- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: PROF. ASSAD ASEMA SIO JAMBO JIPYA OFISI YAKE KUKAGULIWA NA BUNGE
Dar es Salaam: Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali hapa nchini(CAG), Profesa Mussa Assad amesema siyo jambo jipya ofisi yake kufanyiwa ukaguzi, akisema utaratibu huo upo kila mwaka na nimatakwa ya kisheria na taarifa yake baada ya Ukaguzi kuwasilishwa Kamati ya Bunge la Hesabu za Serikali (PAC).
Kauli hiyo ya Profesa Assad ameitoa jana Jumanne Juni 13, 2019 wakati akihojiwa na kituo cha televisheni cha AzamTV
“Tunakaguliwa kila mwaka na mkaguzi wetu kama kawaida atateuliwa na PAC ya Bunge atafanya kazi yake, akimaliza atatoa ripoti na kuitazama sisi na kusainiwa na audit committee halafu hesabu hizo zitapelekwa kwa mwenyekiti wa PAC ili kusoma bungeni.”
“Hayo ni mambo ya kawaida kabisa katika utendaji wa taasisi yetu na siyo jambo jipya, ni matakwa ya kisheria,” alisema Profesa Assad. .
Mei 16, 2019, Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai alitoa taarifa bungeni kwamba kwa mujibu wa sheria ya ukaguzi wa umma, hesabu za ofisi ya CAG zinakaguliwa na Bunge kupitia Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC).
“Hesabu za ofisi ya CAG zinapaswa kukaguliwa angalau mara moja kwa mwaka na Bunge kupitia kamati ya kudumu ya PAC huwa inajukumu la kuteua mkaguzi wa ofisi hiyo.” “Kwa maneno rahisi, Bunge ndiyo tuna tafuta mkaguzi wa nje ambaye anakagua ofisi hiyo,” alisema Spika Ndugai.
CAG PIA alizungumzia bajeti ya Serikali ya mwaka 2019/20 ya Sh33.1 trilioni iliyowasilishwa bungeni Alhamisi iliyopita Juni 13, 2019, akisema, “Kila mwaka baada ya bajeti kupitishwa kazi yetu ni kuhakikisha yale yote yaliyopitishwa na Bunge ndiyo yanayotekelezwa.”
“Kwa hiyo ripoti yetu kwa mwakani itapitia jambo hilo na kutoa maoni pale ambapo yanaonekana yanafaa,” alisema