- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: PROF ASSAD AGOMA KUONDOLEWA KWENYE U-CAG
Dar es salaam. Aliyekuwa Mkaguzi Mkuu na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali, CAG Prof. Mussa Assad amesema hawezi kuzungumza chochote kuhusu uteuzi wa CAG mpya kwa kuwa hana taarifa rasmi Juu ya Uteuzi wake kwa mfumo wa barua kama alivyoteuliwa.
Kwa mujibu wa Taarifa ya Ikulu ya jana na ya leo ya Rais Magufuli inasema kuwa muda wa Prof Assad unaisha leo usiku saa 6 kamaili hivyo kuanzia kesho jumanne anabidi ampishe CAG mpya ambaye ni Charles Kichere.
Akizungumza na kituo cha habari cha DW leo Jumatatu asubuhi Prof Assad amefafanua kuwa, alipoteuliwa alipewa barua ya uteuzi iliyoeleza mambo kadhaa ya kisheria na vifungu vya kisheria kuhusu uteuzi wake, lakini utenguzi huu umekuja bila hata barua ya kueleza chochote kisheria hivyo anaendelea kusubiri huenda akapelekewa barua
Ameongeza kwa, kusema kuwa, ''jambo hili nililitegemea kutokana na mazingira ya kazi yalivyokuwa, lakini Mwenyezi Mungu ndio mtoa riziki, kazi ziko chungu mzima na nilitegemea hii ikiisha nitafanya nyingine hivyo hatuna budi kumshukuru Mwenyezi Mungu''
Kuondolewa kwenye nafasi yake Prof. Assad kama Mkaguzi na Mdhibiti mkuu wa Hesabu za Serekari kumeleta mkanganyiko mkubwa wa kisheria huku watu wengi wakiwemo wanasheria wa kujitengemea sambamba na Wanasiasa wakipinga hatuo hiyo aliyoichukua Rais Magufuli.
Wengi wamekuwa wakisema katiba ya Jamhuri ya Tanzania Ibara 144 inamtaka CAG kudumu Madarakani Mpaka atakapofikisha umri wa miaka 65.