- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: POLISI YAWAKAMATA WANANDOA KWA KUSAMBAZA HABARI ZA CORONA
JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema linawashikilia watu wawili ambao ni mume na mke kwa tuhuma na kueneza taarifa za uongo kwa wananchi kuhusu ugonjwa COVID-19(Corona) na kwamba watafikishwa mahakamani wakati wowote.
Akizungumza leo Machi 27 mwaka 2020 ,Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa amesema watu hao wamekamatwa Machi 20 mwaka huu saa saba mchana wakiwa kwenye daladala aina ya Toyota DCM namba T 119 DKS iliyokuwa ikitokea Muhimbili.
Amewataja watu hao ni Boniphace Mwita na mkewe Rosemary Mwita Mwita kwamba wakiwa kwenye daladala hiyo walianza kupotosha na kutoa kejeli kwa umma kuwa hakuna nchini kwetu hakuna Corona ila Serikali inasema hivyo kwasababu haina fedha na ndio maana imefunga shule kwani wamekosa hela za chakula cha wanafunzi.
Kamanda Mambosasa amesema kuwa kutokana na kejeli na uzushi wa watu hao abiria waliokuwepo ndani ya daladala hiyo walikasirishwa na kuchukua hatua za kuwaweka chini ya ulinzi na kuitaka daladala hiyo ipelekwe Kituo cha Polisi na sasa wanashikiliwa na jeshi hilo kwa ajili ya hatua inayofuata ya kuwapeleka mahakamani.
Amesisitiza kuwa Jeshi la Polisi limeshachukua maelezo ya watuhumiwa hao na jarada tayari wameshapeleka law Wakili wa Serikali kwa ajili ya hatua nyingine za kisheria.
Kamanda Mambosasa ametoa rai kwa Watanzania kutotoa taarifa za kejeli na dhihaka kuhusu ugonjwa wa Corona na kwamba jeshi hilo halitasita kuchukua hatua kwa watakaobainika wanafanya upotoshaji.
" Wenye tabia ya kupotosha kuhusu ugonjwa huu wa Corona waache mara moja, tunashauri wananchi kuendelea kufuata maelekezo yanayotolewa na viongozi wa Serikali pamoja na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto na si vinginevyo,"amesisitiza Kamanda Mambosasa