Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 1:28 pm

NEWS: POLISI YATOA SABABU ZA KUKAMATWA KWA NYALANDU

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) inamshikilia aliyewahi kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu kwa tuhuma za vitendo vinavyoashiria uwepo wa rushwa katika Mkoa wa Singida.
Nyalandu ambaye alihama kutoka Chama cha Mapinduzi CCM kwenda Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) amekamatwa Jumatatu ya leo saa tisa Alasiri mkoani Singida, alihojiwa na TAKUKURU na baadae akapelekwa kuhojiwa na Jeshi la Polisi .

Kwa mujibu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Singida Joshua Msuya amethibitisha kuwa Nyalandu anahojiwa na TAKUKURU kutokana na kufanya vitendo vinavyoashiria uwepo wa rushwa.

"Ni kweli tumemkamata Nyalandu kwa ajili ya kufanya naye mahojiano, kuna mikutano ya kisiasa ambayo wanaifanya na kuna viashiria vya vitendo vya rushwa.

Hivyo tumemkamata kwa ajili ya kumhoji. Tunaomba ifahamike tunamhoji kwasababu ya kuwepo viashiria vya vitendo vya rushwa na si kwamba tumemkamata akitoa rushwa," amesema Msuya.


Alipoulizwa kama bado wanamshikilia au laa ,Msuya amejibu wao baada ya kumhoji wamemkabidhi kwa vyombo vingine vya ulinzi na usalama kwa mahojiano zaidi.

Msuya amesema sio kweli kwamba Nyalandu amevamiwa na watu wasiojulikana wakiwa na silaha, kwa sababu kabla ya kuchukuliwa kwa ajili ya kuhojiwa alipewa taarifa na hivyo alikuwa anajua kuwa anahitajika TAKUKURU.

Lakini kwa upande wao Chama cha Chadema kimesema kuwa Nyalandu alikua kwenye kikao cha ndani pale Itaja Singida Vivijini

" Wamekuja watu wakiwa na silaha za moto, AK47 na SMG. Wakasema wanamtaka Nyalandu, David Jumbe na M/kiti wa Chadema kwenye kata hiyo. Walipoulizwa wao ni nani wakakataa kujitambulisha.

Hata vitambulisho wamegoma kutoa. Wakawashurutisha watu hao watatu hadi kwenye gari na kuondoka nao." alisema mmoja wa Wajumbe waliokuwepo Kwenye kikao.