- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: POLISI YAKIRI KUMSHIKILIA MWANDISHI WA HABARI ERICK KABENDERA
Awali Mkuu wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa alipoulizwa alisema kuwa hana taarifa zozote za tukio hilo, lakini wanafuatilia kupata ukweli kwani ndio kazi yao, na kisha watatoa ufafanuzi hapo baadaye.
Erick Kabendera ambaye ni mwandishi wa habari za kiuchunguzi alichukuliwa kwa nguvu na watu wapatao 6 waliojitambulisha kuwa ni maafisa wa jeshi la polisi nyumbani kwake, Mbweni, Dar es Salaam jioni ya jana Jumatato Julai 29, 2019. Watu hao walimchukua na kusema wanampeleka Kituo cha Polisi Oysterbay, huku wakichukua simu yake na ya mke wake.
Hapo awali taarifa zinasema, kabla ya hapo, simu zake zote zilifungwa; na alipopiga simu Vodacom aliambiwa kuwa hayo ndio maelekezo waliyopewa na Mamlaka ya Mawasiliano ya taifa (TCRA).