Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 12:40 am

NEWS: POLISI WAUSAMBARATISHA MKUTANO WA CUF LIPUMBA

Related image

Dar es salaam: Mkutano mkuu wa Chama cha wananchi CUF upande wa Mwenyekiti anayetambulika na ofisi ya msajili Prof. Ibrahim Lipumba uliokuwa ufanyike katika hotel ya Lekam jijini Dar es salaam umezuiwa kufanyika na Jeshi la Polisi leo Jumanne March 12, 2019 baada ya wajumbe kutoka upande wa Maalim Seif Sharif Hamad kupeleka pingamizi katika Jeshi hilo

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala jijini Dar es Salaam Bw Chembera aliwasili eneo la tukio katika Hoteli ya Lekam na kuwapa taarifa ya kuzua mkutano huo. "Tumekuja kuwaeleza kuhusu zuio hili kwa sababu taaarifa wameshazipeleka makao makuu ya Polisi," amesema Chembera.

Lakini kwa upande wake, Mkurugenzi wa Fedha wa CUF, Thomas Malima na Naibu Katibu mkuu (Bara) Magdalena Sakaya wamesema hawajapata katazo hilo kwa hiyo wataendelea na mkutano.

"Sisi hatujapata hilo katazo, tunaendelea na mkutano," amesema Malima.

Mkurugenzi wa uhusiano wa chama hicho, Abdul Kambaya amesema katazo la Mahakama limewataja watu watatu akiwemo Profesa Lipumba na Magdalena Sakaya. "Katazo limewataja watu watatu, mkutano mkuu unaitishwa na Baraza Kuu, wao watakuja kama waalikwa tu," amesema Kambaya. Muda mfupi, baada ya RPC wa Ilala kuondoka, mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Lipumba aliingia katika eneo la mkutano na kupokelewa kwa shangwe huku akiingizwa kwenye ukumbi ambao waandishi wa habari wamezuiwa kuingia.