Home | Terms & Conditions | Help

November 22, 2024, 1:55 am

NEWS: POLISI WANAODAIWA KUMUUA MFANYABIASHARA MTWARA WABURUZWA MAHAKAMANI

Mtwara. Kesi ya mauwaji inayowakabili Maofisa saba wa Jeshi la Polisi wanaotuhumiwa kumuua mfanyabiashara wa Madini Mkoani Mtwara Mussa Hamis(25) leo wamefikishwa tena katika Mahakama ya Hakimu mkazi Mtwara.

Watuhumiwa hao walifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Januari 25 na kusomewa shitaka la mauaji ya kukusudia lakini Kesi hiyo imehairishwa mpaka Februari 22, 2022 itakapotajwa tena

Akiahirisha kesi hiyo leo Jumanne Februari 8, 2022 Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Lugano Kasebele amesema anaahirisha kesi hiyo kutokana na upelelezi kutokamilika.

Washtakiwa wanaohusishwa na mauaji hayo ni ofisa Upelelezi (OC CID) Wilaya ya Mtwara, Gilbert Kalanje Mkuu wa Kituo cha Polisi Mtwara (OCS), Charles Onyango, Ofisa wa Intelijensia ya Jinai Mkoa wa Mtwara, Charles Kisinza na Mkaguzi wa Polisi, John Msuya pamoja na Mganga Mkuu wa Zahanati ya Marco Mbuta. Wengine ni Mkaguzi wa Polisi, Shirazi Mkupa na Koplo Salimu Juma Mbalu.

Mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Kasebele ilidaiwa kuwa Januari 5 mwaka huu maofisa hao wa polisi walimuua Musa Hamis Hamis (25), mkazi wa Nachingwea mkoani Mtwara.

Kesi ilianza kusikilizwa saa 3:28 asubuhi ambapo Wakili wa Serikali Mwandamizi, Faraja George kwa niaba ya Jamhuri amesema kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika hivyo kuomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa tena.

Hakimu Kasebele amesema kuwa kwa vile upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika hivyo ameahirisha kesi hadi Februari 22, 2022