- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: POLISI WAMSUBIRI LISSU KUFUNGUA KESI YA KUPIGWA RISASI
Mkuu wa Jeshi la polisi nchini Tanzania (IGP), Simon Sirro amesema Jeshi la Polisi halijaweza kumtambua mtu aliyefanya shambulio la risasi kwa Mwanasheria Mkuu wa chama kikuu cha Upinzani Tanzania Chadema na aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu.
amesema ” sisi tunamsubiri Tundu Lissu aje afungue kesi, kitu gani kimetokea, mazingira gani na yule dereva wake. Dereva tunamtafuta imekuwa shida, yeye mwenyewe alipopata matatizo yupo nje hatujamuona, tunamuona tu kwenye mitandao”
Lissu alipigwa Risasi miaka miwili iliyopita nyumbani kwake Area D Jijini Dodoma wakati akiendelea na Majukumu yake ya Kibunge
Katika hatua nyingine IGP Sirro amesema kuwa uchunguzi juu ya kupotea kwa mwandishi wa Habari za uchunguzi, Azory Gwanda wa gazeti la mwananchi unaendelea.
Ameeleza kuwa ameshafungua jalada la uchunguzi, na kuwataka watu kama wantaarifa kuhusu tukio hilo kuzifikisha polisi na si kuishia tu mtandaoni kwani haziwezi kusaidia.
Kamanda Sirro amesema pia kuwa suala la watu kupotea halijaanza leo huku akitolea mfano wa wazee wa kizanaki wengi walikuwa wanasemekana wamepotea lakini baadae wanaonekana.