- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: POLISI SINGIDA WATOA SABABU ZA KUMKAMATA LEMA
Jeshi la Polisi mkoani Singida, limesema limemkamata Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema, kwa ajili ya mahojiano baada ya Mbunge huyo kutoa taarifa zisizo sahihi siku ya Februari 29, 2020, wilayani Manyoni Mkoani Singida.
Kamanda wa Polisi Mkoani humo Sweetbert Njewike, amesema leo Marchi 3, 2020 kuwa bado wanaendelea kumshikilia na uchunguzi ukikamilika watamfikisha mahakamani.
"Tumemkamata baada ya kutoa taarifa zisizo sahihi, kwahiyo tunamhoji na baada ya hapo tutampeleka mahakamani" amesema Kamanda Njewike.
Ofisa Uhamasishaji wa Chadema Mkoa wa Singida, Swaibu Mohamed amesema Lema anatuhumiwa kwa kosa la mtandao. “Lema bado anaendelea kuhojiwa na polisi mbele ya mawakili wake (Amani Mwiru na Hemed Nkulungu),”amesema Mohammed. " kwahiyo tunaendelea kulifutilia swala hili kwa kina kuona wanamfikisha mahakamani au wanamuachia huru"
Jana usiku Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Kanda ya Kaskazini, Aman Golugwa, alitoa taarifa za Mbunge Lema kusafirishwa na Polisi kutoka Arusha hadi Singida kwa ajili ya mahojiano.