- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: POLISI SINGIDA WAMKAMATA MKUFUNZI ALIYEWAZAMISHA ASKARI MAJINI
Jeshi la Polisi Mkoani Singida hatimaye limefanikiwa kumkamata Mkufunzi Msaidizi wa Jeshi la Akiba (Mgambo) Said Ng'imba anayetuhumiwa kutoa adhabu kali kwa Wanafunzi wawili wa Mgambo kwa kuwaambia watumbukie kwenye dimbwi la maji kitendo kilichopelekea kupoteza maisha.
Said Athumani Ng’imba mwenye namba MG129191 alitoa adhabu kwa wanafunzi hao kutokana na kukosa vipindi, vya mafunzo mkufunzi Ng’imba aliwapa adhabu ya kutumbukia kwenye dimbwi lililokuwa limejaa maji na hatimaye wakapoteza hewa na kufariki Duninia.
Wanafunzi waliofariki dunia,ni Emmanuel Hamisi (20) mkazi wa Kijiji cha Mudida na Ismael Hussein (22) mkazi wa Kijiji cha Sepuka.
Wanafunzi hao walikuwa wanahudhuria kozi ya mafunzo ya awali ya jeshi la akiba ambayo yanaendelea kufanyika Kijiji cha Mudida.
“Jeshi la polisi likishirikiana na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, lilifanya juhudi kubwa kuwaokoa,liliwaopoa kutoka majini wakiwa tayari wamefariki dunia.
“Baada ya kutumbukia,walizama ndani ya dimbwi na hawakuonekana,kitendo hiki kilisababisha mkufunzi msaidizi kutimua kusikojulika hadi sasa.Tayari tumeanza kumsaka kwa nguvu na tunatarajia muda si mrefu atakuwa mikononi mwetu,”alisema Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Sweetbert Njewike
Habari kutoka eneo la tukio,zinadai wanafunzi hao kabla ya kutumbukia,walibebeshwa kila mmoja mfuko mgogoni uliojazwa mchanga.