- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: POLISI MTWARA WAZITWANGA WENYEWE HADHARANI
Wakati wananchi mbalimbali hapa nchini wakiomboleza msiba mkubwa wa mfanyabiashara maarufu nchini Dkt Reginald Mengi Askari Polisi na askari wa Jeshi la Magereza wamepigana makonde hadharani katika eneo la stendi kuu ya mabasi barabara kuu iendayo Tunduru, wilayani Masasi Mkoani Mtwara,
Kwamujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Blasius Chatanda, amesema tukio hilo la aina yake lilitokea juzi mawendo wa saa 6 mchana baada ya askari polisi kumkamata askari Magereza ambaye inadaiwa alikuwa anaendesha pikipiki bila ya kuvaa kofia ngumu(helement)
Chatanda alisema baada ya kutokea kwa ugomvi huo, Polisi walifyatua risasi hewani na kurusha mabomu ya machozi hali ambayo ilisababisha taharuki kubwa kwa wananchi wilayani humo. Alisema muda kidogo walitokea askari Magereza watano ambao walifika eneo la tukio kwa ajili ya kumuokoa mwenzao, ndipo polisi na askari wa Magereza walipoanza kupigana.
Kamanda Chatanda alisema polisi huyo alikuwa doria katika operesheni ya kawaida ya ukamataji wa vyombo vya moto hasa pikipiki maarufu kama bodaboda, ambao wamekuwa wakiendesha bila ya kufuata sheria za usalama barabarani.
Alisema baada ya Polisi huyo kumshika askari magereza ambaye alikuwa kiendesha pikipiki bila ya kuvaa kofia ngumu na kumtaka kwenda kituo cha polisi au kuiacha pikipiki yake, alipinga ndipo mzozo ulipoanza.
“Baada ya muda kidogo kundi la askari magereza walifika kumuokoa mwenzao mara baada ya kumuona ameshikwa na Polisi, pia kundi la askari polisi walifika nao kumuokoa mwenzao, ndipo makundi hayo mawili ya jeshi walipoanza kuchapana makonde na kufyatua risasi hewani,” alisema Kamanda Chatanda. Kamanda Chatanda alisema kufuatia tukio hilo, Jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi wa kujua chanzo zaidi ya vurugu hizo ikiwamo kufanya vikao vya dharura kati ya Jeshi la Polisi na Magereza, na kwamba uchunguzi utakapokamilika sheria itachukua mkondo wake.
Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo wakizungumza na Nipashe kwa nyakati tofauti walieleza kuwa waliwaona polisi waliokuwa wamebeba silaha wakimvamia askari magereza ambaye alikuwa amevaa nguo za kiraia akiendesha pikipiki, na kumtaka kuelekea kituoni. Walieleza kuwa askari huyo Magereza alikataa kutii agizo hilo ambapo alitoa maelezo kuwa hawezi kufanya hivyo kwa kuwa yeye ni askari magereza na kwa wakati huo alikuwa kazini hivyo kuondoka bila ya ruhusa ya mkuu wake ni kosa kwake.