- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: POLISI KINONDONI WAMKATAA MAMBOSASA KUKAMATWA KWA TITO MAGOTI
Dar es Salaam. Kamanda wa Polisi Kinondoni (RPC), Dar es Salaam nchini Tanzania, Musa Taibu amesema hana taarifa zozote juu ya kukamatwa kwa ofisa elimu kwa umma wa kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Tito Magoti ndani ya himaya yake.
Taibu amesema licha ya kuwauliza watendaji wake, hakuna mwenye taarifa za kukamatwa kwa ofisa huyo.
Magoti anashikiliwa na Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam tangu Ijumaa iliyopita ya Desemba 20, 2019 baada ya kumkamata akiwa Mwenge Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi wa Kanda hiyo, Lazaro Mambosasa juzi na jana alikiri kuwa wanamshikilia Magoti na wenzake watatu kwa uchunguzi wa tuhuma za makosa ya jinai inayowakabilia
Leo Jumatatu Desemba 23, 2019, Kamanda Taibu akizungumza na waandishi wa habari alizungumzia suala la Magoti baada ya kuulizwa na waandishi hao wakitaka kujua endapo anafahamu ofisa huyo wa LHRC amewekwa kituo gani.
“Kwa bahati mbaya sina taarifa hizi, nimeuliza wenzangu hakuna mwenye taarifa za kukamatwa kwa Tito kwenye himaya yangu.” “Inawezekana amekamatwa kwa siri na mtu mwingine asijue kwa ajili ya kufanikisha jambo fulani na siyo kila jambo linalofanyika lazima polisi ajue inategemea jambo linalozungumziwa ni la aina gani na lina usiri kiasi gani,” amesema Taibu Katika mkutano huo uliokuwa na lengo la kutoa tahadhari kwa wananchi kusherehekea sikukuu ya Krisimasi na mwaka mpya bila kuvunja sheria ambapo amewataka wananchi kuzingatia sheria wakati wa kusherehekea sikukuu hizo.