- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: POLISI HONG KONG WAWAKAMATA WAANDAMANAJI
Polisi wa kuzuwia ghasia katika jimbo la Hong Kong walitumia muda mwingi leo mchana kukabiliana na makundi ya waandamanaji wanaopigania demokrasia waliokuwa wamevalia barakoa wakikusanyika katika maeneo mbali mbali ingawa idadi yao ilikuwa ndogo zaidi na hawakufanya fujo nyingi ikilinganishwa na siku zilizopita.
Maandamano yalifanyika katika maeneo ya karibu huku baadhi ya waandamanaji wakifunga barabara na kurusha vitu katika njia za treni pamoja na kunyunyiza rangi na kuvunja madirisha ya maduka ya wale wanaoiunga mkono China.
Polisi waliwakamata watu kadhaa huku wakijaribu kuwazuwia wanaharakati lakini machafuko hayo hayakuwa makubwa ikilinganishwa na mapema mwezi huu wakati mji huo ulipozongwa na machafuko makubwa kabisa yaliyosababishwa na vuguvugu la maandamano linaloendelea tangu miezi minne iliyopita.