Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 3:38 am

NEWS: POLISI DAR LIMEWATAKA WABUNGE WALIOGOMA KURUDI BUNGENI KUJISALIMISHA

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limewataka wabunge wote walioko Dar es salaam badala ya bungeni Dodoma, wajisalimishe kwa hiari yao katika Ofisi ya Upelelezi ya Kanda Maalum ya Dar es salaam kwa mahojiano.

Hatua Hii ya Jeshi la Polisi ni Baada ya saa 24 zilizotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda kumalizika.

Taarifa hii ya Jeshi la Polisi imetolewa leo Mei 7, 2020 na Kamanda ACP Ronarl Makona kwaniaba ya Kamanda mkuu Kanda maalum ya Dar es salaam.

Jana RC Makonda aliwataka Wabunge wote waliokimbia kushiriki vikao vya Bunge na kwenda Jijini Dar es salaam "kula bata" kuhakikisha wanarudi Bungeni tofauti na hapo watakamatwa kwa kosa la Uzururaji kama wanavyokamatwa machangudoa wanaozurura Usiku.

Alisema Mbunge anaepaswa kuwa Dar es salaam ni yule mwenye Kibali au Ruhusa ya Spika wa Bunge tofauti na hapo ni vyema wakafunga virago vyao na kurudi Bungeni ili kuepuka kukamatwa.

"Hakuna asiefahamu kuwa sasahivi tuko katika Mapambano dhidi ya Virusi vya Corona na sio uzururaji, ifahamike huu sio Mji wa wazururaji hivyo natoa Masaa 24 kwa Wabunge wote kurudi Dodoma tofauti na hapo tutawakamata kwa kosa la Uzururaji kama tunavyowakamata Machangudoa" alisema RC Makonda