- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: POLISI 4 WAUWAWA KWA KUPIGWA RISASI UFARANSA
Polisi wanne wameuawa kwa kupigwa Risasi na Mshambuliaji, ambaye alikuwa miongoni mwa wafanyakazi kwenye makao makuu ya polisi, Shambulio hilo limetokea Alhamisi hii, Oktoba 3 katika makao makuu ya polisi ya Paris, nchini Ufaransa hii ni kwa mujibu wa shirika la habari la AFP.
Shambulio hilo limetokea karibu saa saba mchana ndani ya makao makuu ya polisi jijini Paris, katika eneo la kihistori katikati mwa mji mkuu Paris. Polisi wanne wameuawa. Mtu mwingine amejeruhiwa na yuko katika hali mbaya. Amesafirishwa katika hospitali ya Mafunzo ya Jeshi, Percy.
Hijafahamika wazi jinsi shambulio hilo lilivyotokea. Shambulio liliripotiwa hapo awali katika ofisi ya mshambuliaji, ambaye ni mfanyakazi kwenye makao makuu ya polisi kwa miaka 20. Silaha inayotumiwa katika shambulio hilo ni kisu cha kauri.
Kulingana na ushuhuda wa kwanza uliokusanywa na wanahabari wa RFI, mshambuliaji alikuwa mfanyikazi mzuri.
Waziri wa Mambo ya Ndani Christophe Castaner, Waziri Mkuu Edouard Philippe na Rais Emmanuel Macron wamezuru eneo la tukio. Polisi imezingira eneo hilo.
Wachunguzi wanachunguza uwezekano wa kuwepo mgogoro wa kibinafsi, kulingana na vyanzo vya AFP.