- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: POLISI 2 MBARONI KWA KUMBAMBIKIA MTU KESI
Moshi. Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro limewatia mbaroni askari wake wawili wa kituo cha Polisi cha Himo wilayani Moshi kwa tuhuma za kuandaa jaribio la kumbambikia kesi ya utakatishaji wa fedha, mfanyabiashara Julius Mlay.
Polisi hao na watu wengine watatu, walishinikiza wapewe Sh140 milioni ili wamwachie mfanyabiashara huyo.
Taarifa za uhakika kutoka ndani ya kituo cha Polisi Himo na kituo kikuu Moshi Mjini, askari hao walikamatwa jana kufuatia habari iliyoandikwa na Gazeti la Mwananchi, la nchini Tanzania Januari 6, 2020.
Taarifa hizo zinadai baada ya taarifa hiyo, mkuu wa kituo cha Polisi (OCS) cha Himo alipewa maagizo ya kuwapeleka askari hao makao makuu ya Polisi Kilimanjaro ambako walikamatwa.
Polisi hao walikamatwa Januari 4 na kuandikisha maelezo yao na kisha viongozi wa polisi ngazi ya wilaya wakaingilia kati na kutaka jambo hili limalizwe kidiplomasia.
tokana na makubaliano hayo, polisi hao waliachiwa baada ya kurejesha Sh500,000 kati ya Sh2 milioni na Dola 100 walizompora raia huyo na kuahidi kumalizia zilizobaki mwisho wa mwezi.
Hata hivyo, taarifa zinadai viongozi wa mkoa wa polisi Kilimanjaro hawakuwa wameelezwa ukweli wa tukio hilo, hadi taarifa za tukio hilo zilipofichuliwa na Mwananchi, Januari 6.
Kamanda wa polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Salum Hamduni alipoulizwa jana juu ya sakata hilo alithibitisha kukamatwa kwa askari hao na kwamba wanaendelea kuhojiwa.
“Suala hili tayari limesharipotiwa hapa kituoni na malalamiko yote tumeshayapokea na tunaendelea kuchunguza jambo hili na hao polisi wanaendelea kuhojiwa na jeshi la polisi,” alisema.
Kuhusu watuhumiwa wengine, Kamanda Hamduni alisema wengine waliohusishwa na tukio hilo bado jeshi la polisi mkoani Kilimanjaro linaendelea kuwatafuta.
Taarifa nyingine zinadai watu hao watano si askari polisi bali ni wanaojihusisha na vitendo vya utapeli katika mikoa ya Kilimanjaro na Arusha ikiwamo kujifanya maofisa usalama wa taifa.