Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 3:45 am

NEWS: POLEPOLE AMPONGEZA WAZIRI LUGOLA KWA KUTEMBEA NA ILANI YA CCM

KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole amempongeza kwa kazi nzuri Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola na kumwambia kuwa anachokifanya ni kuunganisha wananchi na Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Lugola ambaye utembea na Ilani ya CCM katika mazingira tofauti ikiwemo ofisini na pamoja na mikutano yake ya kikazi, kitendo hicho kinamfurahisha kiongozi huyo wa CCM na kumtaka achape kazi zaidi.

Polepole alikutana na Lugola Ofisi za CCM Mkoa wa Arusha, leo wakati Waziri huyo alipokua anatoka katika kikao chake na Kamati ya Siasa ya Mkoa ya Chama hicho, alipofanya ziara katika ofisi hizo.

“Mheshimiwa Waziri nakupongeza kwa kuunganisha wananchi na ilani ya CCM, endelea kuchapa kazi,” alisema Polepole. Hata hivyo, Waziri Lugola alimshukuru Polepole kwa kumpa pongezi hiyo na kuahidi kufanya kazi zaidi kwa ajili ya kumsaidia Rais Dkt John Magufuli katika uongozi wake.

Waziri Lugola yupo mkoani humo kwa ziara ya kikazi akifuatilia maagizo yake aliyoyatoa kwa vyombo vya ulinzi na usalama vilivyopo ndani ya Wizara yake.