- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: POLEPOLE AJIKANYAGA KUKIMBIA MDAHALO
DODOMA: KATIBU wa Itikani na Uenezi wa Chana cha Mapinduzi(CCM) Humphrey Polepole,amesema yeye pamoja na viongozi wake hawakuweza kushirika katika mdahalo uliokuwa umeandaliwa na Chadema kwa madai kuwa hawawezi kukaa meza moja na mtu ambaye aliasi chama.
Polepole alisema kuwa viongozi wa CCM wamalanini kuwa mtu yoyote ambaye ameasi chama na kuondoka mwenyewe, hawawezi kukaa meza moja na kuzungumza naye jambo lolote.
Katibu huyo licha ya kutotaja jina la mtu ambaye walionekana kumwogopa katika mdahalo huo lakini alikuwa akimlenga Waziri Mkuu mastaafu wa awamu ya nne Edward Lowassa ambaye alikuwa mwenyekiti katika mdahalo huo pia alikuwa mmoja wa wangombea nafasi ya Urais 2015 ndani ya CCM .
Lowassa alijiengua katika Chama cha Mapinduzi baada ya jina lake kukatwa bila hata kufika tano bora na aliamua kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na Kupewa ridhaa ya kugombea nafasi Urais Kupitia umoja wa katiba ya Wananchi (Ukawa) na kumpa wakati mgumu kwa kutoa ushindani mkali rais wa sasa Dk. John magufuli huku Lowassa akipata kura zaidi ya milioni 6 dhini ya Dk.Magufuli aliyepata kura milioni 8.
“Leo Juzi nimeona kuna kipeperushi kimepita kinasema eti CCM wamekimbia mdahalo, na magazeti kwa wingi wao nao wameandika kuwa sisi tumekimbia mdahalo cha kikubwa kama hiki ninaweza kukimbia mdahalo”alisema Polepole.
“Mimi siwezi kusiwezi kushiriki meza moja na mtu ambaye amekosa na kuvunja miiko ya CCM ,mimi siweza kukaa meza moja na mtu ambaye amevunja miiko na taratibu ndani ya CCM.
“Mimi na viongozi wenzangu hatuwezi kufanya hivyo kwanza hatukuitwa hatukuelezwa mada ni nini pia hata ukumbu ambao waliuandaa walikuwa hawajaulipia sasa sisi na watu tunaowaongoza tujikute tunaondolewa katika ukumbi ambao haujalipiwa hiyo si aibu.
“Pia kama nilivyo tangulia kusema ndani ya Chama tuna taratibu kama mtu anaenda kinyume anaitwa anakanywa na anaendelea na jeuri yake tunamfukuza sasa ikitokea akajitimua mwenyewe sisi hatuwezi kukaa meza moja na mtu huyo akiomba kurudi sawa lakini itamchukua miaka saba kukaa naye mezani ili kuweza kumsikiliza.
“Hata hivyo ifahamike kuwa sisi hatuwezi kukimbia midaharo na hatujakimbia mdaharo bali tumekimbia uovu” alisema Polepole.
Polepole alisema maneno hayo mwishoni mwa wiki alipokuwa akizungumza na shirikisho la wanafunzi wa vyuo vikuu vya Dodoma wakati wa mahafari yao yalioambatana na kukabidhiwa vyeti.
Mbali na hilo Polepole alisema Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kisiwajaribu viongozi wa CCM kwani CCM ina utaratibu wa kuzungumza na si vinginevyo.
Alisema hata utaratibu wa kuwaharika katika mdahalo huo haukufuatwa, kwani ukumbi huo haukulipiwa wala haukufuata utaratibu.
“sisi watu wa serikali ambao tunawasimamia tulisubiri tuondolewe katika ukumbi ambao hata haujalipiwa na fedha ya serikali”alihoji Polepole.
Katika mahafari hayo aliwataka wanavyuo wote waliohitimu kuhakikisha wanaandika majina yao na anwani zao huku akiwataka waelezee na fani zao walizosoma waziwasilishe kwake mapema ili pale inapotokea fursa ndani ya chama na serikalini waweze kupewa kipaumbele kama makada wa CCM.
Akiendelea kuzungumza na wanachuo hao amewapoga marufuku wanavyuo hivyo kutangaza nia ya kugombea nafasi yoyote ndani ya chama hadi pale itakapokuwa umefikia wakati wa kugombea nafasi yoyote ndani ya chama.
Hata hivyo amekiri kuwa ndani ya CCM hususani katika awamu ya Nne CCM ilikuwa imeoza kwa kuwa naviongozi wenye kutenda maovu huku vitendo vya rushwa vikiwa vimeshamili.
“Katika chaguzi ndani ya CCM ilipokuwa ikifikia hatua ya kutangaza nia yapo majitu yalikuwa yakija yanakuambia lazima utuone kama ni mwanaume lazima utoe kitu kidogo na kama ni mwanamke au msichana lazima utoe zaidi ya kitu kidogo kwa maana ya ngono” alisema Polepole.