Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 11:28 pm

NEWS: PETER MSIGWA KUACHIWA KWA DHAMANA.

Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema) Msigwa ameachiwa huru jana usiku kwa dhamana baada ya kukamatwa akiwa kwenye mkutano wa hadhara.


Msigwa aliachiwa baada ya kudhaminiwa na wadhamini wawili Alex Kimbe pamoja na Mwenyekiti wa Bavicha Iringa Leonce Marto , saa nne usiku .


Msigwa alishushwa jukwaani kwa nguvu akiwa anahutubia mkutano wa hadhara katika kata ya Mlandege Manispaa ya Iringa na anatuhumiwa kwa kosa la uchochezi dhidi ya vyombo vya usalama .


Marto amesema mikutano yake imefungiwa na hapaswi kuendelea na ziara yake katika kata nyingine mpaka hapo OCD atakapo amua vinginevyo.


Leo Mbunge anatakiwa kuripoti kwa RCO na huenda kesi ya uchochezi ambayo tayari imeshafunguliwa jalada lake ikapelekwa mahakamani .


Amesema Mbunge huyo atazungumza na vyombo vya habari leo mchana kuweka wazi madhila yaliyompata wakati akitekeleza wajibu wake kwa wananchi.