- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: PAPA FRANCIS " MATUMIZI YA SILAHA ZA KINYUKLIA NI UHALIFU"
Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis ameizuru miji ya Hiroshima na Nagasaki leo na kuyataka madola yenye nguvu kutokomeza hifadhi ya silaha za nyuklia akisema umiliki na matumizi ya silaha hizo ni uhalifu na hatari.
Akiwa amesimama mbele ya wahanga wa mashambulizi ya mabomu ya nyuklia yaliyofanywa na Marekani mwaka 1945, Papa Francis amekemea mwendelezo wa kuvunjika kwa mikataba ya kuzuia umiliki silaha na kuupinga mtazamo wa kulimbikiza silaha kama njia ya kuzuia uchokozi.
Papa Francis amewatolea wito viongozi wa kisiasa duniani kukubali kwamba amani na usalama wa kimataifa utajengwa chini ya msingi wa mshikamano na siyo mazingira ya kutoamaina. Kiongozi huyo ameitembelea miji ya Hiroshima na Nagasaki wakati wa siku ya kwanza ya ziara yake nchini Japan inayonuwia kuhimiza wito wake wa kupigwa marufuku silaha za nyuklia duniani.