- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: PAPA ARIDHIA KUJIUZULU KWA ASKOFU WA TANZANIA
Kiongozi mkuu wa Kanisa la Katoliki duniani, Papa Francis amekubali pendekezo la kutaka kujiuzulu kwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Morogoro nchini Tanznia, Telesphory Mkude sababu kubwa ikielezwa kuwa ni matatizo ya kiafya yanayomsumbua askofu huyo kwa muda mrefu.
Baada ya kukubali Ombi lake la kujiuzulu Papa amemteua Padri Lazarus Msimbe wa Shirika la Mungu Mwokozi maarufu Wasalvatoriani (S.D.S) kuwa Msimamizi wa Kitume wa jimbo hilo ambaye atakuwa akiwajibika moja kwa moja katika masuala yote ya Vatican.
Katika taarifa iliyotolewa na Padri Richard Mjigwa (CPPS) wa Radio Vatican, ilisema Papa Francis ameridhia maombi ya kujiuzulu Askofu Mkude hivyo amemteua Padri Msimbe kuwa Msimamizi wa Kitume jimboni humo.
Askofu Mkude alizaliwa Novemba 30, 1945 Pinde, Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro. Alipata upadrisho Julai 16, 1972 na kuwekwa wakfu na Mwadhama Laurean Kardinali Rugambwa Aprili 26, 1988 kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Tanga ambako alifanya kazi hadi Aprili 5, 1993. Baadaye mwaka 1993, Askofu Mkuu Jimbo Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama Polycap Kardinali Pengo alimweka wakfu kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Morogoro.
Kabla ya uteuzi huo, Padri Msimbe alikuwa ni Makamu wa Shirika la Mungu Mwokozi maarufu Wasalvatoriani. Padri Msimbe alizaliwa Desemba 27, 1963 Homboza mkoani Morogoro. Baada ya masomo yake ya msingi na sekondari, alijiunga na masomo ya falsafa kwenye Seminari Kuu ya Kibosho, Jimbo Katoliki la Moshi. Baadaye aliendelea na masomo ya taalimungu, Seminari Kuu ya Segerea iliyoko Jimbo Kuu la Dar es Salaam. Desemba 8, 1987 kwenye sherehe ya Bikira Maria Mkingiwa Dhambi ya Asili, Padri Msimbe aliweka nadhiri zake za daima na kupewa daraja Takatifu ya Upadri Juni 21, 1998.