- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: ODINGA AWASILISHA KESI MAHAKAMANI KUPINGA USHINDI WA KENYATTA
Nairobi: Mgombea uraisi wa kupitia Muungano wa upinzani nchini Kenya NASA Bw. Raila Odinga amewasilisha kesi ya kupinga ushindi wa Rais Uhuru Kenyatta katika mahakama ya juu Jijini Nairobi.
Msajili wa mahakama ya juu jijini Nairobi Bi Esther Nyaiyaki amekiri kuipokea barua yenye nyaraka za kesi hiyo na ushahidi kutoka kwa mawakili wa muungano huo takriban saa moja na nusu kabla ya muda ulioruhusiwa kutamatika.
Ushahidi na nyaraka zilizowasilishwa mahakamani na upinzani wa NASA zinatajwa kuwa na kurasa elfu tisa.
Tume ya uchaguzi na mipaka nchini Kenya IEBC ilimtangaza raisi Uhuru Kenyatta mshindi wa kiti cha uraisi katika uchaguzi uliofanyika August 8 2017.
Viongozi wa muungano huo wa upinzani wanadai mitambo ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (IEBC) ilidukuliwa na watu wenye uhusiano na serikali ya Jubilee na kwamba watu hao waliingilia na kuchakachua matokeo kumfaa Rais Uhuru Kenyatta aliyekuwa akishindana na Bw Raila Odinga kwa mara ya pili.