- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: NYUMBA YA MSANII PROFESSOR J YABOMOLEWA NA SEREKALI
Dar es salaam: Nyumba ya Mbunge wa mikumi (CHADEMA) na Msanii wa kizazi kipya Joseph Haule alimaarufu Professor J imebomolewa na Tanroad kufuatia nyumba hiyo kuwepo kwenye eneo ambalo hapakustahili kuwepo makazi. Akiandika kwenye Ukurasa wake instagram professor J amesema kuwa yeye nimiongoni mwa wahanga wa bomoa bomoa siku ya tarehe 29 septemba mwaka huu ndipo yumba yake ilibomolewa na Tanroad na ameoneshwa kusikitishwa na uwamuzi huo wa Tanroad.
"Jana nikiwa katika majukumu jimboni Mikumi Majira ya saa kumi mbili hivi jioni, nilitaarifiwa kwamba, watu wa Tanroads wakiwa wameambatana na grader mbili na magari mawili ya polisi (defenders) yenye askari waliokuwa na silaha mbalimbali za moto walikuwa wanabomoa nyumba yangu. (sijawahi kuumia kiasi hiki ) Nimesikitishwa sana jinsi Tanroads wanavyoweza kujichukulia maamuzi bila ya kujali mhimili muhimu wa Mahakama wametoa maagizo gani.
J analalamika kuwa hakuwa na taarifa juu ya ubomolewaji wa nyumba hiyo "Na taratibu zilizotumiwa kubomoa nyumba yangu bila ya mimi na Tanesco kupewa taarifa saa kumi na mbili jioni (haukuwa muda wa kazi) na kubomoa huku Umeme ukiwa unawaka ni kitendo ambacho kwanza kina hatarisha maisha ya wabomoaji wenyewe, maisha ya familia yangu pamoja na majirani zangu , LIMENISIKITISHA zaidi."
Nasema hivi kwasababu Tanesco wamenipigia simu baada ya masaa 24 au zaidi baada ya zoezi la kubomoa nyumba kufanyika kunitaarifu kuja kukata Umeme kabla ya ubomoaji huo, pindi nilipo waambia kwamba mbona nyumba IMESHABOMOLEWA kabisa na sijaweza kuokoa kitu chochote na hata hiyo meter yenu mnayoiulizia mkaitafute kwenye kile kifusi cha nyumba yangu kilichokusanywa kwa pamoja na watu wa Tanroads. Tanesco walishangazwa sana kuvunjwa nyumba yangu kwa taratibu hizo.
Lakini naamini kila kitu kinatokea kwa sababu maalum. Nimejifunza kumtegemea Na kumshukuru Mungu kwa kila jambo. Na hili ni moja ya mitihani ya hapa duniani. Nimepokea na kumsikiliza Mungu ana mipango gani juu yetu katika familia yangu mbeleni. Tumelipokea na Naamini tutashinda alisema mbunge huyo wa mikumi