Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 1:24 am

NEWS: NVUA ZASABABISHA MAAFA SIERRA LEONE

SIERRA LEONE: Idadi ya watu waliopoteza maisha kutokana na maporomoko ya udongo na mafuriko katika mji mkuu wa Sierra Leone, Freetown, imeongezeka na kufikia zaidi ya watu mia tatu.

Inaofiwa kwamba miili zaidi iko chini ya vifusi.

Jitihada za kuokoa zilisitishwa kwa muda baada ya giza kuingia.

Rais Ernest Bai Koroma amesema kupitia televisheni kwamba vituo vya dharura vimewekwa ili kukabiliana na kile alichokiita janga la taifa.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Maporomoko ya udongo

Shirika la Msabala mwekundu limesema inakadiriwa zaidi ya watu laki tatu wamepoteza makazi yao.

Eneo lililoathirika zaidi wilaya ya Regent iliyopo pembezoni mwa mji wa Freetown baada ya mlima uliojaa maji kuporomoka.

#BBCswahili.