- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: NITANYAHU AKATALIWA OMBI LA KUJIUNGA NA UPINZANI
Chama kikuu cha upinzani nchini Israel kimelipinga shauri la waziri mkuu Benjamin Netanyahu la kuunda serikali ya muungano."Hatutojiunga na serikali yoyote pamoja na Netanyahu" amesema Mosche Jaalon ambae ni mwakilishi wa ngazi ya juu wa ushirika wa vyama vya Buluu-Nyeupe.
Kiongozi wa chama hicho Benny Gantz amesema binafsi anataka kuongoza serikali pana ya kiliberali na ya umoja . Benjamin Netanyahu anaonyesha kuvunjika moyo baada ya kukataliwa shauri lake. Hata hivyo anasema yuko tayari kwa mazungumzo.
Baada ya kuhesabiwa asili mia 95 ya kura kufuatia uchaguzi mkuu jumanne iliyopita, matokeo yanadhihirisha hakuna hata mmoja aliyejikingia wingi wa kura kuweza kuunda serikali nchini Israel.