Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 5:44 am

NEWS: NISSAN YATENGENEZA KITI KINACHOWEZA KUGUNDUA JASHO LAMTU

Kampuni ya Nissan yenye maskani yaake Yokohama nchini Japan jana imeuzindua kiti cha gari chenye uwezo wa katambua jasho la mtu, kiti hicho ambacho kampuni hiyo inasema kuwa kitasaidia kupunguza ajali za barabarani.

Kampuni ya Nissan imetengeneza kiti hicho kwa Teknolojia inayojulikana kama Soak, ambacho hubadlisha rangi ikiwa itatambua kuwa dereva atakuwa ameishiwa maji mwilini.

Tafiti za awali zilizofanywa na taasisi za European Hydration Institute na Loughborough University iligundua kuwa madereva wanaoishiwa na maji mwilini huwa na makosa mengi sawa na madereva walevi.

Ngozi hiyo ya kiti iliyoundwa na kampuni moja nchini Uholanzi pia itawekwa kwenye usukani wa gari na viti vya mbele vya gari .

"Hii ni sehemu ya mpango mzima ambao sio tu wa kufuatilia tu gari bali pia dereva." alisema Prof Peter Wells.