Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 10:40 pm

NEWS: NIHF YAIBUKA KIDEDEA MAONYESHO YA 88 DOM

DODOMA: Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NIHF) umeibuka kidedea miongoni mwa mifuko ya hifadhi ya jamii iliyoshiriki maonesho (nanenane ) ya kumi ya kilimo na ufugaji inayoendelea Nzuguni mkoani Dodoma,

Katika maonesho hayo yanayoshirikisha mikoa ya kanda ya kati ya Dodoma na Singida mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) ulishika nafasi ya tatu kwa utoaji wa huduma za hifadhi ya jamii.

Akikabidhi vyeti na zawadi kwa washindi mbalimbali waliofanya vizuri katika maonesho hayo Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mikoa (TAMISEMI),Mh.Selemani Jafo amepongeza jitihada za NHIF na mifuko mingine katika juhudi zao za kumkomboa mtanzania katika nyanja mbalimbali.

“Lengo letu ni kuyafanya maonesho haya ya nane nane hapa Dodoma yawe ya kimataifa,hivyo tunatambua mchango wa washiriki wote katika kumsaidia mkulima na mfugaji,” amesema Mh.Jafo

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti wa NHIF Bi Anjela Mziray amesema tuzo hiyo ni kichocheo kwa mfuko huo katika kuboresha maisha ya Mtanzania.

Akizungumza mara baada ya kupokea cheti maalumu kutoka kwa Mh.Jafo,Bi Anjela Mziray ameshukuru kamati ya maandalizi ya maonesho hayo kwa kutambua mchango wa mfuko wa NHIF.

“Tuzo hii kwetu ni motisha tosha ,na pia itatukumbusha kuwa tuna deni la kuwahudumia Watanznia tulichokionesha kwenye maonesho hayo ndio majukumu yetu ya kila siku,” amesisitiza Bi.Mziray.

Pamoja na hilo Bi Mziray amewataka wakazi wa Dodoma na maeneo ya jirani kutembelea ofisi za NHIF Dodoma zilizopo jengo la hazina ndogo barabara ya UDOM ili kujipatia huduma zinazotolewa na mfuko huo.

Maonesho ya Nane Nane kanda ya kati yalitarajiwa kuharishwa leo lakini kutokana na maombi ya wadau Mh.Jafo ameongeza siku mbili zaidi ili kutoa fursa zaidi kwa wananchi wa kanda ya kati na maeneo jirani kuendelea kupata huduma.