Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 7:32 am

NEWS: NIGERIA YAONGEZA ASILIMIA 50% KIMA CHA CHINI CHA MSHAHARA

Serikali ya Nigeria imeongeza asilimia 50 ya mshahara wa chini, baada ya miezi kadhaa ya mvutano na vyama vya wafanyakazi na vitisho vya mgomo, Waziri wa Kazi Chris Ngige amesema.

Mshahara wa chini katika nchi hii, yenye idadi kubwa zaidi ya watu barani Afrika ni naira 18,000 (sawa na chini ya euro 44) kwa mwezi kwa wafanyakazi katika sekta ya umma na ile ya kibinafsi.

Mnamo mwezi Novemba mwaka jana, wakuu wa Majimbo walifutilia mbali mkataba wa kiwango cha naira 30,000, wakisema "haiwezekani"huku wakipendekeza kupunguzwa kwa watumishi wa umma au kuongeza bajeti wanayotengewa kutoka serikali ya shirikisho.

Licha ya marupurupu ya kila mwezi kutoka serikali ya shirikisho, Majimbo mengi hayajalipa wafanyakazi wao kwa muda wa miezi kadhaa, na kusababisha mdororo wa uchumi kwa taifa hilo kubwa Afrika Magharibi tangu 2016.

Waziri wa Kazi amewaambia waandishi wa habari kwamba jumla ya kiwango cha "(naira) 27,000 kimeidhinishwa", kufuatia mkutano wa Baraza la kitaifa la Majimbo.

Mfumuko wa bei (kwa sasa 11.5%) imekuwa tatizo kubwa nchini Nigeria, nchi inayozalisha kiwango kikubwa cha mafuta barani Afrika, ambapo wakazi wengine kwa jumla ya watu zaidi ya milioni 180 wanaishi katika umasikini.