- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: NIDA YAPIGA MARUFUKU WATU KUOMBWA AFFIDAVIT KITAMBULISHO CHA TAIFA
Dar es salaam: Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) imepiga marufuku utaratibu unaofanywa na baadhi ya Maofisa wa NIDA wasio waadilifu wa kuwaomba wananchi Viambatanisho vingi ikiwemo kuwalazimisha kuleta nakala ya kiapo (Affidavit) ambapo ni kinyume na utaratibu wa NIDA.
Kupitia taatifa yao iliyotolewa leo April 5, 2019 na ofisi ya Vitambulisho vya Taifa NIDA imetaja nakala ya viambatanisho ambavyo mwananchi anapaswa kuwasilisha ili kupatiwa Kitambulisho cha Taifa ni pamoja na Cheti cha kuzaliwa, Kitambulisho cha mpiga kura, Cheti cha shule ya msingi au sekondari, na Cheti cha Udereva.
Viambatanisho vingine ni Kadi ya Bima ya Afya, Kitambulisho cha mzanzibar mkaazi, Cheti cha Ndoa, kitambulisho cha mfuko wa hifadhi ya Jamii, Namba ya Utambulisho ya mlipa kodi (TIN),na Leseni Ya Udereva.
Aidha NIDA imesema Kitambulisho cha Taifa kinatolewa Bure na imewataka wananchi kutoa taatifa ikitokea kuombwa Pesa au Affidavit.