- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: NIDA WATOA RAI KWA WAHAMIAJI KUEPUKA MATAPELI
DODOMA: IDARA ya uhamiaji imesema hati ya kusafiri ni haki ya kila mtanzania ambaye anakidhi vigezo vya kumiliki hatai hiyo.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Afisa Uhamiaji mkoa wa Dodoma,Peter Kundy,alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika viwanja vya maonesho ya wakulima na wafugaji Nanenane kanda ya kati yaliyofanyika kwenye viwanja vya nzuguni mjini Dodoma.
Kundy amesema kuwa licha ya kuwa hati ya kusafiria ni haki ya kila mtanzania lakini mwananchi huyo ni lazima awe amekidhi vigezo vinavyomfanya kukubaliwa kuwa na hati hiyo.
Hata hivyo amesema wananchi wanatakiwa kuwa makini na baadhi ya watu ambao ni matapeli wanaojifanya kuwa ni maafisa uhamiaji kwa kujidai kuwa wanaweza kutoa hati hizo kwa muhitaji.
Amesema hati za kusafiria hupatikana katika ofisi za idara ya uhamiaji na kwa kujaza fomu maalumu ambazo kwa sasa zinapatikana kwa tovuti ya idara ya uhamiaji.
Akizungumza na waandishi wa habari amesema Idara ya Uhamiaji inafanya kazi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutoa elimu kwa jamii juu ya utoaji wa taarifa kwa watu ambao wanaweza kuwa wahamiaji haramu.
Amesema licha ya Tanzania kuwa kichochoro cha wahamiaji haramu ambao ujipenyeza kwa ajili ya kupita kwenda katika nchi ya Afrika idara hiyo inaendelea kupambana kwa lengo la kuthibiti hali hiyo.
Amesema mapambano hayo yanaatokana na kutoa elimu kwa jamii kuanzia ngazi ya kitongoji,kijiji, kata,tarafa,wilaya,mkoa hadi taifa ili jamii itambua madhara ya kuwa na wahamaji haramu.
Wakati huo huo mamlaka ya utoaji wa vitambulisho vya uraia (NIDA) imesema kuwa ifikapo 30 Desemba mwaka zoezi la usajili wa watanzania wote kwa ajili ya kuwapatia vitambulisho vya uraia litakuwa limekamilika.
Akizungumza na waandishi wa habari Afisa usajili Mkoa wa Dodoma,Khalid Mrisho, amesema zoezi hilo linaendelea vizuri licha ya kuwepo kwa changamoto za hapa na pale.
Changamoto alizozitaja ni pamoja na kuwepo kwa mkanganyiko wa watu ambao wakati mwingine taarifa zao hazijakaa vizuri na kushindwa kujilikana kama ni raia au la.
Hata hivyo amewataka wananchi kuhakikisha taarifa zao na kuchukua fomu za usajili ili waweze kupatiwa vitambulisho vyao vya uraia hapo baadaye.