- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: NGO'MBE ASABABISHA AJALI MOJA AFARIKI DUNIA SITA KUJERUHIWA.
Watu sita kujeruhiwa na moja kupoteza maisha huku watu zaidi ya 50 wakinusurika kifo baada ya ajali iliyosababishwa na ng'ombe aliyekuwa akivuka barabara ghafla bila kuonekana na dereva wa basi la kampuni ya Kidia One.
Ambapo basi hilo lililokuwa linatokea Dar kwenda Mwanza.
Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo Kaimu Kamanda wa Polisi SSP Elias Mwita Mkoa wa Shinyanga amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambaopo amesema ajali hiyo imetokea eneo la tinde nyuma kidogo kabla ya kufika Mkoa wa Shinyanga.
Akielezea mazingira ya ajali hiyo Kaimu Kamanda Mwita amesema ng'ombe alitokeza na kuvuka barabara ghafla huku ikidaiwa kuwa dereve alikuwa hajamuona na alipomuona alikuwa akijitahidi kumkwepa hali iliyosababisha apoteze uelekeo na kupelekea gari kupinduka na kusababisha kifo pamoja na majeruhi.
Hata hivyo Kamanda Mwita amesema majeruhi sita wapo hospitali wakipatiwa matibabu lakini dereva ametorokea kusikojulikana ingawa wanaimani kama Jeshi la polisi hadi kufikia leo mchana watakuwa wameshamkamata.