- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: NETANYAHU MBIONI KUPOTEZA NAFASI YAKE
Matokeo ya awali katika uchaguzi wa Israel yanaonyesha kuwa Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu na wapinzani wake wa siasa za kidini na kizalendo wameshindwa kupata idadi ya kutosha ya wabunge katika uchaguzi wa Jumanne.
Hii inatoa nafasi kwa mazungumzo ya kuunda serikali ya muungano jambo ambalo huenda likauweka hatarini mustakabali wa kisiasa wa waziri huyo mkuu na kusafisha njia yake kufunguliwa mashtaka kwa madai ya ufisadi.
Matokeo ya awali yaliyotolewa na vituo vitatu vikuu vya Israel yameonyesha kuwa mpinzani mkuu wa Netanyahu Benny Gantz na chama chake cha Samawati na Nyeupe akiongoza kwa viti 32 vya ubunge mbele ya chama cha Likud cha waziri huyo mkuu kilicho na viti 30. Bunge la Israel lina wabunge 120. Huku matokeo hayo yakiwa hayaashirii kwamba Gantz ndiye atakayekuwa waziri mkuu mpya, yanaonyesha kuwa Netanyahu ambaye ameiongoza Israel kwa miaka kumi atakuwa na wakati mgumu sana kuendelea na kazi hiyo.
Akiwahutubia wafuasi wake, Gantz amesema watashinikiza kubuniwa kwa serikali ya muungano huku Netanyahu naye akisema ni bora kusubiri matokeo rasmi yatakapotoka.
Matokeo ya awali katika uchaguzi wa Israel kwa kawaida huwa si ya uhakika na huku matokeo rasmi yakitarajiwa kutolewa Jumatano, huenda bado Netanyahu akapata ushindi, ingawa vituo vyote vitatu vimeonyesha matokeo sawa.
Huku ikiwa hakuna anayeweza kupata idadi kubwa ya wabunge kati ya Netanyahu na Gantz bila uungaji mkono wa Avigdor Lieberman aliyekuwa katika serikali ya waziri mkuu huyo, Lieberman ameebuka kama mshindi wa kweli, kwani kuna uwezekano mkubwa kwamba yeye ndiye atakayeamua atakayejumuishwa katika serikali ijayo.
Akiwahutubia wafuasi wake Lieberman alisema "tuna njia moja tu: serikali pana ya muungano na ya kiliberali itakayoundwa na chama cha Yisrael Beitenu, Likud na Smawati na Nyeupe."
Wabunge katika chama cha Gantz pia wameelezea uungaji mkono wao wa serikali ya muungano ambayo huenda ikajumuisha wadhfa wa waziri mkuu ambao utakuwa unazunguka kwa watu tofauti.