Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 8:21 pm

NEWS: NETANYAHU AELEKEA KUPATA USHINDI MWEMBAMBA

Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu anaonekana kushinda katika uchaguzi wa nchi hiyo hatua inayomuweka katika nafasi ya kuunda serikali ya muungano Huku asilimia 97.4 ya kura zikiwa zimeshahesabiwa, matokeo ya uchaguzi huo uliofanyika jana Jumanne yanaonesha kuwa chama cha Likud cha Netanyahu na washirika wake wa kisiasa kimepata ushindi wa viti 65 katika bunge la Israel lenye viti 120 na bila shaka chama hicho kitakuwa kwenye nafasi ya kuunda serikali ijayo ya muungano ya mrengo wa kulia.

Israel Wahlen Wahlparty Netanjahu (picture-alliance/AP Photo/A. Schalit)

Hii itakuwa mara ya tano kwa Netanyahu kuiongoza Israel na hatua hiyo inamuweka katika nafasi ya kuwa waziri mkuu aliyeiongoza Israel kwa muda mrefu zaidi baadae mwaka huu na kumshinda David Ben-Gurion muasisi wa taifa hilo.

Likud na Blue and White zafungana

Chama cha Likud kinaonekana kupata idadi sawa ya viti bungeni na chama hasimu cha Blue and White muungano unaofuata siasa za wastani ambao unaongozwa na aliyekuwa mkuu wa majeshi, Benny Gantz. Netanyahu na Gantz wote wamedai kushinda katika uchaguzi huo. Waziri Mkuu Netanyahu amesema amefurahishwa na ushindi huo mkubwa na kwamba tayari ameanza kuzungumza na washirika wake watakaounda serikali ya muungano.

Chama chake cha Likud kinaonekana kupata idadi sawa ya viti bungeni, kama hasimu wake katika uchaguzi huo mkuu wa zamani wa jeshi Benny Gantz anayeongoza muungano wa vyama vya siasa za wastani wa rangi ya Bluu na nyeupe.Lakini wakati asilimia 97 ya kura zikiwa zimekwisha hesabiwa, matokeo yanaonesha Likud na vyama vingine vya mrengo wa kulia ambavyo ni washirika wake vikiwa na viti 65 katika bunge lenye viti 120.