Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 4:18 pm

NEWS: NEEMA YASHUKA VIJANA WAPEWA FURSA YA KUTOA MAPENDEKEZO KUTATUA TATIZO LA UKOSEFU WA AJIRA

DODOMA: Serikali imeingia katika awamu ya pili ya kukusanya mapendekezo ya maboresho ya sera ya Taifa ya maendeleo ya vijana ya mwaka 2007 ambapo vijana wametakiwa kutoa mapendekezo yatakayosaidia sera hiyo kuleta mabadiliko chanya yatakayoondoa tatizo sugu la ukosefu wa Ajira kwa vijana nchini.

Lengo la kufanya mapitio ya maboresho ya sera ya taifa ya maendeleo ya vijana ni kuandaa mazingira rafiki ya sekta ya vijana nchini yatakayoshirikisha vijana katika maendeleo na kukuza uchumi wa nchi na kuondokana na matatizo ya ukosefu wa Ajira kwa vijana pamoja na ukosefu wa mitaji

Akizungumza wakati wa kongamano la kupitia maboresho ya sera ya vijana na kuunda rasimu ya kwanza ya sera mpya lililowakutanisha vijana kutoka mikoa mbalimbali nchini katibu mkuu idara ya kazi ofisi ya waziri mkuu Eric Shitindi amewataka vijana kutumia fursa kutoa mapendekezo yatakayoondoa tatizo sugu la ukosefu wa Ajira

Baadhi ya vijana walioshiriki katika kongamanao hilo wamesema tatizo la ajira, kukosa ujuzi,mitaji na kutoaminiwa ni kikwazo kikubwa kwa kundi hilo kushiriki katika mipango mbalimbali ya maendeleo ya taifa

Naye mkurugenzi wa maendeleo ya vijana kutoka ofisi ya waziri mkuu James Kajugusi amesema sera iliyopo ina zaidi ya miaka 10 na inakabiliwa na mabadiliko makubwa hivyo serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo ya vijana pamoja na vijana wenyewe wameona ipo haja ya kuleta sera mpya itakayoendana na mabadiliko yaliyopo sasa.

Takwimu zinaonyesha kuwa idadi ya vijana katika nchi zinazoendelea kama Tanzania inaendelea kukua kwa kasi sana na hivyo kuongezeka kwa vijana wengi wasio na ajira na wenye hali duni ya maisha, ukosefu wa mitaji, ukosefu wa mbinu jumuishi na kukosa fursa za kiuchumi