Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 12:57 pm

NEWS: NECTA YASOGEZA MBELE MTIHANI WA KIDATO CHA 6

Dar es Salaam. Baraza la Mitihani nchini Tanzania (Necta) limetangaza kuahirisha mitihani yote ya kidato cha sita na Mitihani ya ualimu iliyokuwa ifanyikwe Mei 4 mwaka huu 2020 hadi pale itakapotoa taarifa mpya.

Image result for NECTA tanzania

Kupitia maagizo hayo Necta imetoa maelekezo kwa maofisa elimu wa wilaya kuwajulisha wakuu wa shule na vyuo vya ualimu nchini wawajulishe watahiniwa kuhusu kuahirishwa kwa mitihani hiyo.

Taarifa hiyo ya Necta imekuja baada ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kutangaza Machi 17, 2020 kufungwa shule zote za awali, msingi na sekondari hadi kidato cha sita pamoja na vyuo vya ualimu ili kuondoa misongamano na kupambana na virusi vya ugonjwa wa corona.

Image result for NECTA tanzania

Majaliwa pia aaliagiza ufanyike utaratibu kwa ajili ya wanafunzi waliotakiwa kufanya mitihani ya kidato cha sita na ualimu Mei 4, 2020.

Vile vile, Majaliwa pia Machi 18 aliagiza kufungwa kwa vyuo vikuu nchini ikiwa ni njia ya kupunguza maambukizi ya virusi vya corona ambayo hususani kwenye misongamano ya watu wengi.