- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: NEC YAONGEZA SIKU 3 ZA KUJIANDIKISHA DAR ES SALAAM
TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imeongeza siku tatu katika Zoezi la Uboreshaji Daftari la Wapiga Kura katika mkoa wa Dar es Salaam, zoezi hili lilitangazwa kuwa litadumu kwa siku 7 kuanzia Tarehe 14 hadi tarehe 20 mwezi Februari mwaka huu, tarehe ambayo ni leo.
Akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam, Dk. Wilson Mahela, Mkurugenzi wa Uchaguzi NEC, amesema hatua hiyo imechukuliwa baada ya tume hiyo kufanya tathimini ya zoezi hilo, na kubaini kwamba kuna uhitaji wa siku kuongezeka
Amesema, zoezi hilo lililoanza tarehe 14 Februari mwaka huu litakoma rasmi tarehe 23 Februari 2020, na kwamba baada ya siku hizo kuisha, muda hautaongezwa tena. “NEC katika kikao chake kilichofanyika jana tarehe 19 Februari 2020 ilifanya tathimini ya zoezi la uboreshaji daftari la wapiga kura linaloendelea Dar es Salaam, kwa kutumia mamlaka iliyopewa chini ya kifungu cha 15 kifungu kidogo cha kwanza cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi.
Tume imemua na kuelekeza kuwa, muda wa zoezi hilo liongezwe kwa siku tatu. Sasa litakamilika tarehe 23 , zoezi la litanedelea hadi siku ya Jumapili katika vituo vyote vya Dar es Salaam, vituo vitendelea kufunguliwa saa 2 asubuhi na kufunguliwa saa 12 jioni,” amesema Dk. Mahela.
Dk. Mahela amesihi wakazi wa Dar es Salaam kutumia vyema ongezeko la siku hizo, ili kuhakikisha wanahuisha taarifa zao katika daftari hilo, kwa ajili ya kupata fursa ya kupiga kura kwenye Uchaguzi Mkuu wa Mwezi Oktoba mwaka huu. “Tume inawasishi wananchi wa Dar es Salaam kutumia muda huu vizuri uliongezwa ili kuhakikisha taarifa zao zinaingizwa katika daftari, kwa kuwa hakutakuwa na muda wa nyongeza katika awamu ya kwanza ya uboreshaji daftari, watumie nafasi hii vizuri wajitokeze kwa wingi. Kadi yako ni kura yako nenda kajiandikishe,” amesema Dk. Mahela.