- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: NDUGULILE AMEWATAKA WAUGUZI KUTOWANYANYAPAA WAGONJWA
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile amewataka watumishi wote wa afya nchini kuendelea kupokea wagonjwa wanaokabiliwa na magonjwa ya msingi ukiwemo Ugonjwa unaosumbua kwasasa nchini na Dunia wa Covid-19, sambamba na kupatiwa huduma na Matibabu kama wana maambukizi ya ugonjwa huo.
“Watumishi wenzangu wa afya nawaomba msiwanyanyapae wagonjwa, wapatieni huduma hasa wenye magonjwa mbalimbali,” amesema Dkt. Ndugulile.
Naibu Waziri ametoa kauli hiyo leo Aprili 5, 2020 wakati alipokuwa akikagua Jengo la Maabara ya kisasa ya Kupasua Ubongo lililopo MOI jijini Dar es salaaam, huku akiwataka wataalamu wa afya kujilinda katika sehemu za kazi dhidi ya maambuikizi ya Covid-19 kwa kuwa kipaumbele cha Serikali ni kuwalinda watumishi wa afya ili waweze kuwahuduma wagonjwa.