Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 3:46 am

NEWS: NDUGU WA RUGE WAOMBA MSAADA, MATIBABU YAKE NI MIL 5 KWA SIKU

Dar es Salaam: Ndugu wa mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji wa Clouds Media Group Ruge Mutahaba wameomba msaada wa fedha kwa ajili ya kulipia gharama za matibabu za ndugu yao, huku wakieleza kuwa matibabu yake ni ghali sana kuyamudu wao kama familia au Ruge Mwenyewe.

Akizungumza katika mahojiano na kituo cha Televisheni cha Clouds jana Jumatatu, Februari 18, Kaka wa Mkurugenzi huyo Mbaki Mutahaba alisema kwa sasa Ruge anapatiwa matibabu Afrika Kusini ambako kwa siku gharama ni Sh5milioni. "Alianza kuumwa Mwezi wa 3 mwaka 2018 baada ya kutoka kwenye fursa, alilazwa katika Hospitali ya Kairuki kisha akapelekwa India, sapoti ni kubwa tunashukuru na hata Rais (John Magufuli) ametoa mchango na anaendelea, "alisema Mbaki Mutahaba

"Ana figo ambayo haipo sawasawa ilikuwa lazima wambadilishe. Madaktari wa hospitali ya Kairuki na Muhimbili wakashauri apelekwe Afrika Kusini maana ni karibu zaidi lakini gharama ni kubwa." Ameongeza, "Kule (Afrika Kusini) mfumo wao wa malipo ni tofauti unapaswa kulipa fedha taslimu.

Mbaki amesema kuwa inaonekana hali ya figo ya Mkurugenzi huyo madaktari wanaonekana wanaweza kuhumudu hali hiyo, lakini kazi kubwa iliyobaki ni kumfanyia rehab ili aweze kurikava

Kuna namba rasmi imeandikishwa kwa jina la mdogo wetu Kemilembe Mutahaba unaweza kutusaidia." Namba hiyo ni 0752 222210 kwaa maana ya mchango wako