- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: NDEGE YA KENYA YAUWA WATU 6 BAADA YA KUANGUKA
Watu sita wamepoteza maisha katika ajali ya ndege ya mizigo ya kenya iliyoanguka Jumatatu nchini Somalia, wakati ilikuwa ikisafirisha vifaa vya kupambana na Corona, wizara ya mambo ya nje ya Kenya imesema Leo Jumanne Mei 5, 2020.
Kulingana na gazeti la kila siku la Daily Nation, ndege hiyo ilidunguliwa na watu wasiojulikana.
viongozi wa Kenya wameomba Somalia kufanya uchunguzi kuhusu "mazingira ya tukio hilo" ambalo "halieleweki".
Ndege hiyo ya kibinafsi ya mizigo kutoka Kenya- Embraer 120 - ilikuwa imesheheni vifaa kama sehemu ya mapambano dhidi ya janga la Corona wakati ilipoanguka Jumatatu alasiri katika wilaya ya Bardale Kusini mwa Somalia, wizara ya mambo ya nje ya Kenya imebaini.
Watu sita walio katika ndege hiyo iliyokuwa ikifanya safari fupi kutoka Baidoa kwenda Bardale, kilomita 300 Kaskazini Magharibi mwa mji mkuu wa Somalia, Mogadishu, walipoteza maisha, mamlaka imesema.
"Ndege ilikuwa karibu kutua kwenye uwanja wa ndege wa Bardale wakati ilianguka na kuwaka moto. Watu sita waliokuwemo katika ndege hiyo walifariki dunia katika ajali hiyo," afisa wa polisi katika eneo hlilo Abdulahi Isack ameliambia kwa simu shirika la habari la AFP.
Kundi la Al-Shabab lina ngome zake Kusini mwa Somalia, lakini eneo ambalo ajali hiyo ilitokea huko Bardale liko chini ya himaya ya serikali na kikosi cha jeshi la Umoja wa Afrika kutoka Ethiopia lililotumwa kusimamia amani nchini Somalia.
Meja Jenerali Mohammed Tessema, msemaji wa jeshi la ulinzi la kitaifa la Ethiopia, amesema hana taarifa kuhusu ajali hiyo.
Wizara ya Uchukuzi na Anga ya Somalia imesema katika taarifa kwamba "inahuzunishwa atukio hilo" na kwamba serikali itafanya "uchunguzi wa kina".
Wizara hiyo imeongeza kuwa ndege hiyo iilikuwa ikitumiwa na shirika la African Express, lenye makao yake makuu jijini Nairobi.
Kulingana na Daily Nation, marubani wote wawili walikuwa ni raia wa Kenya na watu wengine wanne walikuwa raia wa Somalia.